Visitors Counter

»Today   119               
»Week   119               
»Month   321               
==============
»Total  23307551        

ANGALIZO KWA WAOMBAJI WA NAFASI ZA KAZI

July 4, 2017


Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwasisitizia waombaji wote kusoma kwa makini tangazo la nafasi za kazi na kuzingatia sifa za msingi na maelekezo yaliyotolewa kabla ya kutuma maombi ikiwemo kuthibitisha (Certify) Nyaraka (Vyeti) pamoja na kuweka sahihi (Signature) katika barua ya maombi ya kazi ambayo imeainisha nafasi inayoombwa.

Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya kielektroniki katika “recruitment portal” http://portal.ajira.go.tz ya Sekretarieti ya Ajira.


Watakaoenda kinyume na malekezo hayo, maombi yao hayatashughulikiwa.

 
Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Sekretarieti ya Ajira.