Call for Interview

Placements

Visitors Counter

»Online   67        
»Today   1012       
»Yesterday  4113       
»Week   9382        
»Month   111582       
==================
»Total 21582991        

Wahitimu wa Vyuo vikuu wapewa elimu kuhusu utaratibu wa Ajira Serikalini.

May 22, 2017


Sekretarieti ya ajira katika Utumishi wa umma imeendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa Vyuo mbalimbali nchini kuhusu utaratibu wa mchakato wa ajira Serikalini kwa lengo la kuwajengezea uelewa na uwezo wa masuala yanayohusu mchakato wa ajira katika utumishi wa umma.

Akizungumza katika mahafali ya Jumuiya ya wanafunzi wa Taasisi za Vyuo vikuu Tanzania (TAHILISO) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki  Katibu msaidizi wa Sekretarieti hiyo Bibi Khadija Isihaka ameeleza kuwa, wahitimu wa vyuo vikuu ni moja ya wadau wakubwa wa Sekretarieti ya ajira ambao wanapaswa kujua utaratibu wa ajira Serikalini na namna ya kutuma maombi ya kazi pindi nafasi wazi zinapotangazwa.

“Katika Utekelezaji wa majukumu ya Sekretarieti ya ajira, wahitimu wa Vyuo vikuu ni wadau  muhimu kwetu, hivyo ni wajibu wetu kuwapa uelewa kuhusu utaratibu wa ajira katika Utumishi wa Umma” alisema Isihaka.

 

Katika mahafali hayo wahitimu hao walipata fursa ya kujua mambo mbalimbali yanayohusu utaratibu unaotumika kutuma maombi ya kazi kwa njia ya kielektroniki ‘Recruitment portal’, uandaaji wa  wasifu binafsi (CV), umuhimu wa kuambatanisha nyaraka muhimu kama vyeti vya kitaaluma wakati wa kutuma maombi yao ya kazi na mambo muhimu wanayopaswa kuzingatia wakati na kabla ya usaili.

 

Katika halfa hiyo, wahitimu kutoka vyuo mbalimbali walipata fursa ya kujua majukumu ya Sekretarieti ya Ajira na umuhimu wa kufungua akaunti kwenye mfumo portal ya ajira unaopatikana kwa anuani ya https://portal.ajira.go.tz kwa ajili ya kuingiza taarifa zao zitakazowasaidia kuwasilisha maombi ya kazi katika mfumo huo pindi zinapotangazwa.

 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa umma, 22 Mei, 2017.