Advertised Posts

Visitors Counter

»Today   149               
»Week   149               
»Month   44195               
==============
»Total  23266372        

KUONGEZWA MUDA WA KUWASILISHA MAOMBI YA KAZI KWA NAFASI YA MHUDUMU WA JIKONI NA SANITARY HAND II.

April 10, 2018


Waombaji kazi wa fursa za Ajira kwa nafasi za Mhudumu wa Jikoni (Kitchen Mess Attendant) kwa tangazo la MDA’s na Sanitary Hand II ya Taasisi ya Elimu Kibaha ambayo mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 11/4/2018 wanaarifiwa kuwa muda wa kutuma maombi yao ya kazi umeongezwa hadi tarehe 24 Aprili, 2018.

Muda huo umeongezwa baada ya kubaini wapo waombaji wenye sifa za msingi wanaoshindwa kutuma maombi yao ya kazi kutokana na mfumo wa Ajira kuwatambua waombaji kazi wenye elimu kuanzia ngazi ya cheti ambao wameingiza taarifa zao na kufikia asilimia 70 ambayo huwawezesha kuwasilisha maombi ya kazi.

Kutokana na changamoto hiyo mfumo umefanyiwa maboresho ambapo sasa waombaji kazi wa kada hizo ambao sifa za kuingilia ni elimu ya kidato cha  4 (form four) wanatakiwa kujaza taarifa zao na ikifikia  kuanzia asilimia 38 wataweza kutuma maombi ya kazi bila shida yeyote.

Muda huu ulioongezwa utahusu kada hizo mbili tu, nafasi nyinginezo katika matangazo hayo muda wa uwasilishaji utaendelea kuwa ule ulioainishwa katika tangazo la kazi. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliokuwa umejitokeza hapo awali.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.