Taarifa kwa Umma.

August 9, 2016


Hivi Karibuni Serikali ilitoa taarifa kwa umma kuwa Ajira zimesitishwa kwa muda ili kupisha zoezi linaloendelea la uhakiki wa watumishi Serikalini. Aidha Sekretarieti ya Ajira pia ilitoa taarifa ya kuahirishwa kwa usaili wa nafasi za kazi kwa tangazo lililotolewa tarehe 1 Juni, 2016 hadi hapo mtakapoarifiwa tena.

Pamoja na taarifa ambayo Sekretarieti ya Ajira iliiyoitoa, bado imekuwa ikipokea maswali kutoka kwa wadau mbalimbali hususan waombaji kazi wakiulizia ni lini mchakato wa ajira utarejea.

Kwa taarifa hii tunawataarifu kwa mara nyingine kuwa Serikali bado inaendelea na ukamilishaji wa zoezi la uhakiki wa watumishi na mara baada ya zoezi hilo kukamilika taarifa itatolewa na Mamlaka husika, hivyo mnaombwa kuendelea kuvuta subira.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, 9 Agosti, 2016.