MABADILIKO YA RATIBA YA USAILI KWA KADA YA MAAFISA BIASHARA II (TRADE OFFICER II).

November 28, 2017


Waombaji kazi wa nafasi ya Afisa Biashara Daraja II walioitwa kwenye usaili wa Mchujo uliopangwa kufanyika tarehe 2 Desemba 2017 katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na tarehe 7 Desemba, 2017 kwenye usaili wa Mahojiano, wanajulishwa kuwa usaili wa kada hiyo umesogezwa mbele hadi tarehe 16 Desemba, 2017 kwa usaili wa Mchujo na tarehe 20 Desemba, 2017 katika usaili wa Mahojiano.

Waombaji kazi wote walioitwa kwenye nafasi ya Afisa Biashara Daraja la II wanaombwa kuzingatia mabadiliko hayo.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kufuatia mabadiliko hayo.

 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.