Call for Interview

Placements

Visitors Counter

»Today   1438               
»Week   1438               
»Month   29199               
==============
»Total  23379585        

Wadau wa Sekretarieti ya Ajira watakiwa kutumia vizuri Madhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kupata huduma.

June 22, 2018


Wadau wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma  wametakiwa kutumia vizuri nafasi iliyotolewa na Serikali ya kuwa na wiki ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutembelea Ofisi za Sekretarieti ya Ajira ili kuweza kupata ufafanuzi wa jambo lolote linalohusu  uendeshaji wa Mchakato wa Ajira serikalini. 

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi amesema  hayo leo alipokuwa akiongea na baadhi ya wadau waliomtembelea ofisini kwake wakitaka kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu mchakato wa Ajira. Amesema Ofisi za Sekretarieti ya Ajira Dar es Salaam na Zanzibar ziko wazi kwa kipindi chote cha maadhimisho haya ambayo yameaanza tarehe 16 Juni, 2018 na yanatarajiwa kumalizika tarehe 23 Juni mwaka huu.

"Unapoongelea Ajira unaongelea maisha ya watu, hivyo, kutokana na umuhimu huo, mimi na watumishi wenzangu tumejipanga kuendelea kukutana na wadau wote watakaojitokeza na wale watakaopenda kuwasiliana nasi kwa njia mbalimbali ikiwemo simu za kiganjani ama mitandao ya kijamii ili kuweza kupokea maoni yao, kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali watakayouliza kulingana na majukumu yaliyokabidhiwa kwa chombo hiki kuyatekeleza. Hivyo niwaombe wananchi wote na wadau kutumia fursa hii vyema ili kuweza kupata majibu sahihi ya kile wanachotaka kukifahamu" alifafanua Daudi.

Amesema  anawakaribisha  Wananchi na Wadau  wote wanaotaka kuonana nae. Aidha,  kwa upande wa Zanzibar  atakuwa huko  tarehe 21 na 22 Juni, 2018 kuanzia saa mbili asubuhi katika Ofisi zao zilizopo Shangani.

Hata hivyo, Sekretarieti ya Ajira imetoa fursa kwa wadau ambao hawataweza kutembelea Ofisi zao  na kutoa maoni ama kuuliza swali bado wanaweza kupiga simu namba 0784-398259 / 0687- 624975 au kuandika kile wanachokitaka kupitia anwani zifuatazo; malalamiko@ajira.go.tz, gcu@ajira.co.tz, facebook.com/psrsajira, twitter.com/psrsajira na Instagram psrsajira ambapo yatajibiwa papo hapo.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Mapambano dhidi ya Rushwa kwa kushirikisha wadau na kujenga uongozi bora ili kufikia malengo ya Ajenda 2063 ya umoja wa Afrika na Malengo ya Maendeleo endelevu”