Call for Interview

Placements

Visitors Counter

»Today   1440               
»Week   1440               
»Month   29201               
==============
»Total  23379587        

TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.

June 14, 2018


Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoanza tarehe 16-23 Juni, 2018 imejiandaa kukutana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu na ufafanuzi wa hoja na maswala mbalimbali  juu ya utekelezaji wa majukumu yake. Sekretarieti ya Ajira tumekuwa tukipokea Maoni/maswali/hoja mbalimbali zinazohusu uendeshaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma.

Katika maadhimisho ya mwaka huu 2018 Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwakaribisha wadau na wananchi wote kuwa kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni, 2018 ambao wangependa kutembelea ofisi za Sekretarieti ya Ajira ili kupata ufafanuzi kuhusiana na majukumu yanayotekelezwa na taasisi hiyo kwa kuwa  itakuwa ikitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira zilizopo Dar es Salaam katika Jengo la Maktaba Kuu ya Taifa ghorofa ya pili na Ofisi ya Sekretarieti ya Ajira Zanzibar zilizopo Shangani mkabala na African House Hotel kuanzia saa 8:30 asubuhi hadi saa 10:30 jioni.

Aidha, kwa wananchi ambao hawatapata fursa ya kutembelea Ofisi zetu wanaweza kuwasilisha hoja/ maoni/maswali kwa kupiga simu katika namba zifuatazo na kuongea moja kwa moja na Watendaji wa Sekretarieti ya Ajira ili kupata majibu ama ufafanuzi wa hoja/maswali yao kwa kupiga simu 0784-398259 au 0687- 624975, Pia wanaweza kutuma ujumbe mfupi kupitia anwani zifuatazo; malalamiko@ajira.go.tz, gcu@ajira.co.tz, facebook.com/psrsajira, twitter.com/psrsajira na Instagram psrsajira ambapo yatajibiwa papo hapo.

Imetolewa na;

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, 14 Juni, 2018.