Call for Interview

Placements

Visitors Counter

»Today   1483               
»Week   1483               
»Month   29244               
==============
»Total  23379630        

Frequently Asked Questions


Kwa kawaida Sekretarieti ya Ajira mara baada ya kuwapangia vituo vya kazi Waombaji wa fursa za ajira waliofaulu usaili hutoa majina katika Tovuti pamoja na kuwatumia wahusika barua za kwenda kuripoti katika vituo vya kazi kwa kupitia anuani zao walizokuwa wameandika katika barua za kuombea kazi.

Aidha, hutoa fursa ya kuchukua nakala ya barua kwa waombaji ambao huamua kuja kuifuata ofisini baada ya kuona imechelewa kuwafikia au wanaojua anuani wanazotumia sasa ni tofauti na zile za awali huku wakiwa na kitambulisho cha kuweza kuthibitisha kuwa yeye ndio mhusika wa hiyo barua.

Kuhusu kwa nini barua haimfikii mhusika kunaweza kusababishwa na mwombaji kubadili anuani na kutokutujulisha na sisi kutuma katika anuani ya zamani au mhusika kuandika kimakosa anwani yake na mwisho mhusika kutokwenda kufuatilia katika sanduku lake la barua (posta) au sehemu alioyokua ameandika.

Endapo mhusika ataona hapati barua yake baada ya kupita siku saba hadi kumi na nne (7-14) tangu kutolewa kwa tangazo la kuitwa kazini na sababu zilizotolewa hapo juu hazimuhusu basi atupigie simu kwa namba 255-687624975 kwa maelezo zaidi.

Kwa kawaida Sekretarieti ya Ajira mara baada ya kuwapangia vituo vya kazi Waombaji wa fursa za ajira waliofaulu usaili hutoa majina katika Tovuti pamoja na kuwatumia wahusika barua za kwenda kuripoti katika vituo vya kazi kwa kupitia anuani zao walizokuwa wameandika katika barua za kuombea kazi. 


Aidha, hutoa fursa ya kuchukua nakala ya barua kwa waombaji ambao huamua kuja kuifuata ofisini baada ya kuona imechelewa kuwafikia au wanaojua anuani wanazotumia sasa ni tofauti na zile za awali huku wakiwa na kitambulisho cha kuweza kuthibitisha kuwa yeye ndio mhusika wa hiyo barua.


Kuhusu kwa nini barua haimfikii mhusika kunaweza kusababishwa na mwombaji kubadili anuani na kutokutujulisha na sisi kutuma katika anuani ya zamani au mhusika kuandika kimakosa anwani yake na mwisho mhusika kutokwenda kufuatilia katika sanduku lake la barua (posta) au sehemu alioyokua ameandika.


Endapo mhusika ataona hapati barua yake baada ya kupita siku saba hadi kumi na nne (7-14) tangu kutolewa kwa tangazo la kuitwa kazini na sababu zilizotolewa hapo juu hazimuhusu basi atupigie simu kwa namba 255-687624975 kwa maelezo zaidi.

 

Tunashukuru kwa swali lako. Ila napenda kulijibu kama ifuatavyo; ni kweli kipindi cha hivi karibuni tulikumbana na tatizo la baadhi ya watu ambao waliamua kuupotosha Umma wa Watanzania kwa kuchukua matangazo yetu yalilopita ambayo yalitolewa kipindi cha nyuma na kuyafanyia marekebisho na kuyatoa tena katika baadhi ya  mitandao yao ya kijamii hususani "eastafricajobscareer.com". Endapo utakuwa umefuatilia utaona katika mtandao wetu pamoja na Vyombo vingine vya habari tulitoa taarifa rasmi ya kukanusha matangazo hayo na kuwataka watu wote wenye kutafuta ajira Serikalini pindi wanapoona matangazo ya kazi yameandika Sekretarieti ya Ajira wajiridhishe kwanza kabla ya kutuma maombi kwa kutembelea Tovuti yetu maana ni lazima tutakuwa tumeweka tangazo husika.


Tunapenda kuwatangazia wadau wetu wote kuwa Sekretarieti ya Ajira haihusiki na matangazo hayo ya kughushi yanayowekwa katika mtandao huo wa www(dot)eastafricajobscareer(dot)com. Hivyo, inawataka waombaji wote wenye kutafuta kazi pamoja na wadau wetu kuyapuuza matangazo hayo kwani ni ya kughushi na yana lengo la kuwasumbua pamoja na kuwaingiza katika gharama zisizokuwa na msingi. 


Kutokana na hilo Sekretarieti ya Ajira inawaomba wadau wetu wote pindi wanapoona matangazo ya nafasi za kazi Serikalini wajiridhishe kwa kuyathibitisha kama ni ya kweli kwa kuangalia katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira au kuwasiliana nasi kwa njia zifuatazo Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kwa Barua pepe; gcu@ajira.go.tz  au Simu; 255-687624975.

a) Sehemu ya kwanza kuhusu kada ya Afisa Maendeleo ya vijana ambayo ilitangaza nafasi 15 lakini wakaajiriwa 9, ukweli ni kwamba wakati nafasi hizi zinatangazwa tulikuwa na matarajio ya kupata vibali vya ajira 15 lakini baada ya usaili kwisha vibali ambavyo vilikuwa vimepatikana ni 9 ndio maana idadi ikawa hiyo, hivyo wasailiwa wengine ambao walifaulu katika kada hiyo wamehifadhiwa kwenye Kanzidata na mara baada ya nafasi za kazi kupatikana watapangiwa kulingana na utaratibu.


b) Kada ya Community Development Officer ambayo waliitwa kazini watu zaidi ya 50 wakati zilizotangazwa zilikuwa 12 hii inatokana na ukweli kuwa wakati nafasi hizo zikitangazwa zilikuwa 12 lakini baada ya hapo vibali viliongezeka kulingana na mahitaji kutoka kwa waajiri yaliyowasilishwa kabla ya waombaji kuitwa kwenye usaili hivyo ilibidi waombaji kazi wote wenye sifa kuitwa kwenye usaili na ndio maana hata waliopangiwa vituo vya kazi walikuwa zaidi ya nafasi 12 zilitangazwa awali.

Tunashukuru kwa maswali yako, Sekretarieti ya Ajira imeanzisha utaratibu kwa waombaji wote wa maombi ya kazi kutumia mfumo wa kuwasilisha maombi ya kazi kwa njia ya mtandao katika ‘Recruitment Portal’, Unaweza kujiunga na mfumo huu wakati wowote kuanzia sasa maana huwezi kuwasilisha maombi yako ya kazi bila kujiunga na mfumo huo, utaratibu wa kujiunga  unapaswa uwe tayari unayo barua pepe kisha fungua portal ya ajira yaani portal.ajira.go.tz ili ujisajili na kuingiza taarifa zako za kitaaluma na nyinginezo. Aidha, unashauriwa kufungua Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ili kuweza kusoma na kufahamu hatua kwa hatua namna ya kujisajili kwa kuwa maelekezo yametolewa kwa mapana na marefu ili kupata muongozo mzima utakaokuwezesha kutambua namna ya kujisajili katika mfumo huo kwa kubonyeza sehemu iliyoandikwa ''Recruitment Portal''

Ni kweli inawezekana umejaza detail zote sasa tatizo la system kutokubali ni kwa sababu profile yako haijafikia asilimia 70, Hivyo,unatakiwa kurejea kwenye portal sehemu ya Academic Qualifications na kuhakiki kama utakua umeweka vyeti vyote, hakiki vyeti vyako kimoja baada ya kingine unaweza kukuta baadhi ya vyeti hujaviambatisha kwenye mfumo. Endapo tatizo hilo litaendelea tafadhali usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0687624975 kwa maelekezo zaidi.

Jibu/ufafanuzi

Kulingana na swali lako kipengele (a) ni vyema kuthibitisha nyaraka zako kwa mwanasheria au mahakamani kwa kuwa baadhi ya waombaji wamekuwa wakitumia nyaraka za kughushi kuwasilisha maombi ya kazi. Aidha, hata mnapozituma pia tumekuwa na utaratibu wa kuziwasilisha nyaraka hizo kwa mamlaka husika ambapo waombaji wa kazi wamedai kuzipata na baadhi yao zimeweza kugundulika ni za kughushi. Pia kwa kuwa serikali hutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu endapo muhusika atakuwa amewasilisha nyaraka ambazo si halisi na halali na tunamashaka nazo tuweze kumchukulia hatua za kisheria kwa haraka. Ni matumaini ya Sekretarieti ya Ajira kwamba wewe na wadau wengine mnafahamu madhara ya kuajiri watu wasio na sifa ya taaluma walioisomea.

Endapo cheti cha kuhitimu elimu ya ngazi husika mfano shahada, au stashahada kimeshatoa kutoka chuoni huitaji kutumia ''Trascript'' tena utawasilisha nakala ya cheti peke yake wakati wa kutuma maombi ya kazi, ila siku ya usaili utapaswa kuja na cheti halisi kwenye usaili wa mchujo kama utakuwepo au usaili wa mahojiano (Oral Interview) kwa ajili ya uhakiki. Tumekuwa tukikubali kupokea maombi ya kazi yaliyowasilishwa kwa kutumia ''Trascript'' kwa kuwa vyeti vya wahitimu husika unakuta havijatoka wakati tangazo la kazi limetangazwa.

Jibu

 

Kwa kuwa tayari Baraza la Mitihani (NECTA) walishatuma taarifa zako Sekretarieti ya Ajira ukiitwa kwenye usaili mwingine huhitaji kulipia tena gharama hizo kwa kuwa tayari taarifa za upotevu wa cheti chako tunazo. Utakachotakiwa kufanya ni kutujulisha kuwa umepotelewa na cheti husika na ulishawasiliana na mamlaka husika taarifa zako zilishatumwa kwetu na sisi tutalihakikisha hilo na kama ni kweli utaruhusiwa kufanya usaili kama kawaida. Nyaraka za Serikali zina utaratibu wake wa kuhifadhi kulingana na mahitaji ya taarifa husika.

Answer.

Yes, we admit that there are some applicants who apply for more than one post, then it happens for them to attend multiple Interviews because they have applied more than one post as well due to their qualifications and its their right to be selected for interview. Also they are free to choose to do both interview if time allows or to do where he is more comfotable and likely easier for him or her to get it. So if he qualified  for both Jobs its just the decision for The PSRS board to decide which Job to be offered to the particular applicant based to appropriate qualifications which he/she has for that post. Usually the Board through its mandate awards the candidate the most senior post or the one he/she passed (scored higher).

Answer.

You will be employed to the first Job (Senior Accountant) because you have passed and it was first interview you did before the other one. So automatically it will affect the second Interview (Chief Accountant) because by that time you will be placed somewhere already. Otherwise if the first placement was done and then some few days later before reporting to the  employer you realize that you have qualified the other interview (Chief Accountant) you may contact PSRS to request if you can be placed to the higher position (Chief Accountant) so that Senior Accountant position can be given to someone else who is qualified. 

Answer.

As you might be aware that the mandate of doing recruitment in the government is given to the Secretariat as it states in the Public Service (Amendment) Act, 2007 Section No.29 (1) that the Secretariat is supposed to facilitate recruitment of employees in the Ministries, Independent Departments, Executive Agencies (MDAs) and other Public Institutions. One of the core functions of the Secretariat is to interview various applicants for various posts, and this function involve preparations interview and examination questions that will be used during the interview depending on the nature of the post. 

The role of the Secretariat when they are switched by other independent boardies varies depending on the nature of Institutions.The roles vary from being an observer, experts and check and balance, though to most organization like Universities the main accountability remains to them.

Answer.

In the scenario where the interviewee feels that the interview conducted by you or by another government organization was anyhow unjust/Unfair; is there any mechanism through which an interviewee can launch kind like complaints? Is there any mechanism to look through the process to determine the truth about the doubts of the interviewee? Otherwise, you are doing a great job, keep it up; I know you will reach your goals.Thank you in advance.

Thanks for your compliment for what were doing. Coming to your question yes, there are mechanisms where you can forward your complains if you have an evidence that somewhere  something is not right which was done during the recruitment by Secreatariat or other Public Institution. First, for us you can submit to the Secretary of Public Service Recruitment Sectretariat and if you are not satisfied with the responses you can send your complains to the Secretary of Public Service Commission or you can send to the Permanent Secretary of the Public Service Management for further action, It is adviced to follow the already set mechanisms for your complains or appeals.

 Jibu

 

Barua za kupangiwa vituo vya kazi hutumwa posta mara baada ya tangazo la wanaoitwa kazini kuwekwa kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira. Pia tumekuwa na utaratibu wa kutoa fursa kwa wasailiwa walioshinda usaili ambao wako jijini Dar es salaam na wale wa mikoa ya karibu na wangependa kuchukua barua zao kwa mkono ofisini kwetu ndani ya siku tatu mara baada ya tangazo kutolewa ili kuwaepushia usumbufu kwa kuwa baadhi yao wamekuwa wakilalamika kuwa wanatumia masanduku ya ndugu na nyakati nyingine ndugu wanakuwa safarini au unakuta masanduku hayajalipiwa hivyo kukosa huduma. Baada ya kipindi hicho kupita barua zote hupelekwa posta kwa kutumwa kwa wahusika. Aidha, kwa baadhi ya Wizara na Taasisi zimekuwa zikichukua barua na taarifa nyingine za msingi ili kuweza kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na wasailiwa walioshinda usaili ambao wamepangiwa katika wizara na taasisi zao. 

Jibu.

 

Asante kwa swali lako, tunakushauri ufungue portal (portal.ajira.go.tz) kisha fungua sehemu uliyoandikwa Register ili uweze kuingiza email yako na namba ya siri kisha baada ya hapo kafungue barua pepe yako yako kawaida na ujumbe utakayokuta kwenye imbox yako ufungue kwa ajili ya ‘Activation’(kama hutakuta ujumbe huo kwenye inbox fungua sehemu iliyoandikwa ‘Spam’) baada ya hapo utakua umeingia kwenye mfumo na kuanza kujaza taarifa zako kadri mfumo unavyokuelekeza na ukikwama wasiliana nasi tafadhali.