MABADILIKO YA RATIBA YA USAILI WA MAHOJIANO (ORAL INTERVIEW)

Posted on October 13, 2017 at 02:01 PM

Waombaji kazi walioitwa kwa ajili ya Usaili unaotajariwa kufanyika kuanzia tarehe 14 - 21 Oktoba, 2017 wanafahamishwa kuwa kutakuwa na mabadiliko ya tarehe ya usaili wa mahojiano (Oral Interview) kwa baadhi ya nafasi mbalimbali zilizotangazwa.  Mabadiliko hayo yatawahusu baadhi ya wasailiwa waliokuwa waanze usaili wa Mahojiano kuanzia tarehe 16, 17, 18 Oktoba, 2017 kwa taasisi za Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa (MOI), Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) na Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) watatakiwa kuongeza siku moja mbele kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. 

Read More

Posted on October 5, 2017 at 10:59 AM

HOTUBA YA MHESHIMIWA ANGELLAH J. KAIRUKI (MB) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA 

BORA) KWENYE UZINDUZI WA BODI YA TATU YA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA ULIOFANYIKA KATIKA WA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA, TAREHE 5 OKTOBA, 2017

 

Read More

MAJINA YA WASAILIWA WANAOITWA KWENYE USAILI WA MAJOHIANO KWA KADA YA DEREVA II

Posted on September 27, 2017 at 09:00 PM

Wasailiwa wa kada ua Udereva waliofanya usaili wa vitendo (Practical) na kufaulu wanatakiwa kufika kwenye usaili wa mahojiano utakaofanyika katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira-Maktaba Kuu ya Taifa-Dar es Salaam, siku ya Jumanne tarehe 03-10-2017.

Wasailiwa wakumbushwa kufika na vyeti vyao vyote pamoja na Leseni ya uendeshaji Gari. (Tafadhali bonyeza 'READ MORE' hapa chini kupata majina)

Read More

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Posted on August 24, 2017 at 11:51 AM

Serikali katika mwaka wa fedha uliomalizika 2016/2017 iliahidi kutoa Ajira serikalini zaidi ya 52,000 kwa Watanzania, ambapo katika siku za hivi karibuni Serikali imekuwa ikitoa vibali vya kuajiriwa watumishi wa kada mbalimbali ikiwemo Waalimu wa Sayansi, Kada za Afya na maeneo mengine kulingana na mahitaji.

Read More

ANGALIZO KWA WAOMBAJI WA NAFASI ZA KAZI

Posted on July 4, 2017 at 11:57 AM

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inapenda kuwasisitizia waombaji wote kusoma kwa makini tangazo la nafasi za kazi na kuzingatia sifa za msingi na maelekezo yaliyotolewa kabla ya kutuma maombi ikiwemo kuthibitisha (Certify) Nyaraka (Vyeti) pamoja na kuweka sahihi (Signature) katika barua ya maombi ya kazi ambayo imeainisha nafasi inayoombwa.

Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya kielektroniki katika “recruitment portal” http://portal.ajira.go.tz ya Sekretarieti ya Ajira.

Read More